[65.1] Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basiwapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyenihisabu ya eda. Na mcheni Mwenyezi Mungu, Mola wenuMlezi. Msiwatoe katika nyumba zao, wala wasitokewenyewe, ila wakifanya jambo la uchafu ulio wazi. Hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu,msiikiuke. Na mwenye kuikiuka mipaka ya MwenyeziMungu, basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui; labdaMwenyezi Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya.
[65.2] Basi wanapo fikia muda wao, ima warejeeni muwawekekwa wema, au farikianeni nao kwa wema. Na mshuhudishemashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.Hivyo ndivyo anavyo agizwa anaye muamini MwenyeziMungu na Siku ya Mwisho. Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea.
[65.11] Mtume anaye kusomeeni Aya za Mwenyezi Mungu zinazobainisha, ili kuwatoa walio amini na wakatenda memakutoka gizani kuwapeleka kwenye nuru. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na akatenda mema,atamwingiza katika Bustani zipitazo mito kati yake,wadumu humo milele. Mwenyezi Mungu amekwisha mpariziki nzuri.