[7.37] Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, au anaye zikanushaIshara zake? Hao itawafikia sehemu yao waliyoandikiwa, mpaka watakapo wafikia wajumbe wetukuwafisha, watawaambia: Wako wapi mlio kuwa mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema:Wametupotea! Na watajishuhudia wenyewe kwamba walikuwamakafiri.
[7.38] Mwenyezi Mungu atasema: Ingieni Motoni pamoja naumma zilizo pita kabla yenu za majini na watu. Kilautakapo ingia umma utawalaani wenzake. Mpaka watakapo kusanyika wote humo, wa mwisho wao watawasema wamwanzo wao: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio walio tupoteza;basi wape adhabu ya Motoni marudufu. Atasema: Itakuwa kwenu nyote marudufu, lakini nyinyi hamjui tu.
[7.43] Na tutaondoa chuki vifuani mwao, na mbele yao iweinapita mito. Na watasema: Alhamdulillah! Kuhimidiwani kwa Mwenyezi Mungu, ambaye aliye tuhidi kufikia haya. Wala hatukuwa wenye kuhidika wenyewe ingeli kuwaMwenyezi Mungu hakutuhidi. Hakika Mitume wa Mola wetuMlezi walileta Haki. Na watanadiwa kwamba: Hiyo ndiyoPepo mliyo rithishwa kwa sababu ya mliyo kuwamkiyafanya.
[7.53] Je, lipo wanalo lingojea isipo kuwa matokeo yake?Siku yatapo fika matokeo yake watasema wale waliokisahau: Kweli Mitume wa Mola Mlezi wetu waliletaHaki! Je, tunao waombezi ili watuombee? Au turudishweili tufanye yasiyo kuwa yale tuliyo kuwa tukiyafanya?Bila ya shaka wamejikhasiri nafsi zao, na yamewapotea waliyo kuwa wakiyazua.
[7.54] Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kishaakatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwamchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, nanyota zinazo tumika kwa amri yake. Fahamuni! Kuumba naamri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, MolaMlezi wa viumbe vyote.
[7.57] Na Yeye ndiye anaye peleka pepo (za kuvuma) kuwani bishara kabla ya kufika rehema yake. Hata hizo pepozinapo beba mawingu mazito tunayachunga mpaka kwenye nchi iliyo kufa. Kisha tunateremsha kwayo maji, ndiokama hivyo tukatolesha kila aina ya matunda. Basi halikadhaalika tunavyo wafufua wafu, ili mpate kukumbuka.
[7.73] Na kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Saleh.Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu.Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwisha kukufikieni Ishara iliyo wazi kutoka kwa Mola wenuMlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye niIshara kwenu. Basi mwachieni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru, isije kukushukieniadhabu chungu.
[7.85] Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yaoShua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni MwenyeziMungu. Hamna mungu mwengine isipo kuwa Yeye. Imekwishakufikieni hoja wazi kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Basitimizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunjewatu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika nchi, baada ya kuwa imekwisha tengenea. Hivi ndivyo borakwenu ikiwa nyinyi ni Waumini.
[7.89] Bila ya shaka itakuwa tumemzulia uwongo MwenyeziMungu tukirudi katika mila yenu baada ya kwisha tuokoanayo Mwenyezi Mungu. Wala haiwi kwetu sisi kuirejea mila hiyo, ila akitaka Mwenyezi Mungu, Mola Mleziwetu. Ujuzi wa Mola Mlezi wetu umeenea katika kilakitu. Kwa Mwenyezi Mungu tunategemea. Ewe Mola Mleziwetu! Tuhukumie baina yetu na kaumu yetu kwa haki,nawe ndiye mbora wa wanao hukumu.
[7.143] Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Molawake Mlezi akamsemeza, alisema: Mola wangu Mlezi!Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahalapake basi utaniona. Basi alipo jionyesha Mola Mleziwake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipo zindukana alisema:Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wakwanza wa Waumini.
[7.146] Nitawatenga na Ishara zangu wale wanao fanyakiburi katika nchi bila ya haki. Na wao wakiona kilaIshara hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu hawaishiki kuwa ndiyo njia; lakini wakiiona njia yaupotofu wanaishika kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababuwamezikanusha Ishara zetu, na wameghafilika nazo.
[7.150] Na alipo rudi Musa kwa watu wake, nayeamekasirika na kuhuzunika, alisema: Ni maovu yaliojemlio nifanyia nyuma yangu! Je, mmeitangulia amri yaMola wenu Mlezi? Na akaziweka chini zile mbao, naakamkamata kichwa ndugu yake akimvutia kwake. (Haarun) akasema: Ewe mwana wa mama yangu!Hakika hawa watu wamenidharau, na wakakaribia kuniuwa.Basi usiwafurahishe maadui juu yangu, wala usinifanye pamoja na watu madhaalimu.
[7.155] Na Musa akawateuwa watu sabiini katika kaumu yakekwa miadi yetu. Na ulipo fika mtetemeko mkubwaalisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ungeli taka ungeliwahiliki wao na mimi zamani! Unatuhiliki kwa waliyoyafanya wajinga katika sisi? Haya si chochote ila nimtihani wako, umpoteze umtakaye na umhidi umtakaye.Wewe ndiye Rafiki Mlinzi wetu. Basi tughufirie nauturehemu. Na Wewe ndiye mbora wa kughufiria.
[7.157] Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiyesoma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katikaTaurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na anawaharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao naminyororo iliyo kuwa juu yao. Basi wale walio muamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na wakaifuatanuru iliyo teremshwa pamoja naye - hao ndio wenyekufanikiwa.
[7.158] Sema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume kwenunyinyi nyote, niliye tumwa na Mwenyezi Mungu Mwenyeufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mungu ila Yeye anayehuisha na anaye fisha. Basi muaminini Mwenyezi Munguna Mtume wake asiyejua kusoma na kuandika, ambayeanamuamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili mpate kuongoka.
[7.160] Na tuliwagawanya katika makabila kumi na mbili,mataifa mbali mbali. Na tulimfunulia Musa walipomuomba maji watu wake kumwambia: Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako. Mara zikatibuka humo chemchem kumi nambili, na kila watu wakajua mahali pao pa kunywea. Natukawafunika kivuli kwa mawingu, na tukawateremshia Manna na Salwa. Tukawaambia: Kuleni vizuri hivitulivyo kuruzukuni. Wala hawakutu- dhulumu Sisi, baliwamejidhulumu wenyewe.
[7.169] Na wakafuatia baada yao kizazi kibaya walio rithiKitabu. Wakashika anasa za haya maisha duni, nawakasema: Tutasamehewa! Na ikiwajia tena anasa kamahiyo wataishika pia. Je, hawakufanyiwa agano la Kitabukuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila Haki tu? Naowamekwisha soma yaliomo humo. Na nyumba ya Akhera nibora kwa wanao jikinga na maasi. Basi je, hamtiiakilini?
[7.176] Na tungelitaka tungeli mtukuza kwa hizo Ishara,lakini yeye aliushikilia ulimwengu na akafuata pumbaolake. Basi mfano wake ni mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi na ukimwacha pia hupumua nakutoa ulimi. Huo ni mfano wa kaumu wanao zikanushaIshara zetu. Basi simulia hadithi, huendawakatafakari.
[7.187] Wanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini?Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu.Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye. Ni nzitokatika mbingu na ardhi. Haikujiini ila kwa ghafla tu.Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema:Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini aghlabu yawatu hawajui.
[7.189] Yeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; nakatika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae nayekwa utulivu. Na anapo muingilia hubeba mzigo mwepesi, akitembea nao. Anapo kuwa mja mzito, wote wawilihumwomba Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wao: Kama ukitupamwana mwema tutakuwa katika wanao shukuru.