[73.20] Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika weweunakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusuyake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayeukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuwekahisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur'ani. Anajua ya kuwa baadhi yenuwatakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhiwakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyosomeni kilicho chepesi humo, na mshike Sala, na toeniZaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenumtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, naina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenyekusamehe Mwenye kurehemu.