[74.31] Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika,wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanishawalio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwena shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapatekusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndiokama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, nahumwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya sichochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu.