The Muslims Internet Directory
SURAT AL-MURSALAAT
Home ↓
Directory ↓
Quran ↓
Hadith ↓
Virtual Library ↓
Discover Islam ↓
Gallery ↓
Webmasters ↓
Dictionary ↓
Downloads ↓
Kids/Games ↓
Login/Register ↓
Quran Tools
Quran Books
Quran Translations
Search
Downloads
Index
Audio
More Links
Muslims Internet Directory
The Quran
The Hadith
2Muslims.com
The Internet
Our Network
Islamic Library
Help/FAQ
Help?
2Muslims Services
Feature Your Site
Submit Your Site
Islamic IE Toolbar
Interactive Games
Free Guestbook
Islamic Internet Gadgets
Islamic Quizzes
Islamic CGI Scripts
Zakat Calculator
Send a Postcard
Islamic Date Converter
DAWA Tools
FAQ About Islam
Hijab
Why do muslim females wear Hijab (Head cover)?
Faith
Culture
Fear
Other
Results
Other Polls
Home
:
Quran Translations
:
Swahili
: Swahili Translation: SURAT AL-MURSALAAT
--Select language--
Albanian
Arabic
Azerbaijani
Bengali
Bosnian
Brazilian
Burmese
Dutch
English_Abdullah_Yusuufali
English_Hasan_Qaribullah
English_Muhammad_Pickthall
Farsi
Finish
French
German
Hausa
Hindi
Hindi
Indonesian
Italian
Japanese
Korean
Latin
Malaysian
Melayu
Meranao
Mexican
Pashto
Persian
Poland
Portuguese
Russian
Spanish
Swahili
Tamil
Thai
Transliteration
Turkish
Urdu
Advance search options
[77.1] Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!
[77.2] Na zinazo vuma kwa kasi!
[77.3] Na zikaeneza maeneo yote!
[77.4] Na zinazo farikisha zikatawanya!
[77.5] Na zinazo peleka mawaidha!
[77.6] Kwa kuudhuru au kuonya,
[77.7] Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
[77.8] Wakati nyota zitakapo futwa,
[77.9] Na mbingu zitakapo pasuliwa,
[77.10] Na milima itakapo peperushwa,
[77.11] Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,
[77.12] Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
[77.13] Kwa siku ya kupambanua!
[77.14] Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ninini?
[77.15] Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
[77.16] Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
[77.17] Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?
[77.18] Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
[77.19] Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
[77.20] Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
[77.21] Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
[77.22] Mpaka muda maalumu?
[77.23] Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
[77.24] Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
[77.25] Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
[77.26] Walio hai na maiti?
[77.27] Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenyekuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
[77.28] Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
[77.29] Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
[77.30] Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
[77.31] Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
[77.32] Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
[77.33] Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
[77.34] Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
[77.35] Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
[77.36] Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
[77.37] Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
[77.38] Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeninyinyi na walio tangulia.
[77.39] Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
[77.40] Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
[77.41] Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli nachemchem,
[77.42] Na matunda wanayo yapenda,
[77.43] Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwamkiyatenda.
[77.44] Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendaomema.
[77.45] Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
[77.46] Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi niwakosefu!
[77.47] Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
[77.48] Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
[77.49] Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
[77.50] Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?
Bookmark Us
-
Set as Home
-
Terms Of Use
Other Sites
:
Know The Prophet campaign
-
Discover Islam
-
Links SQL Plugins
Copyright 2003-2013
Islamic Education & Services Institute
: Murfreesboro, TN