[8.41] NA JUENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums(sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya MwenyeziMungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, nawasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu natuliyo yateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo,siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Munguni Muweza wa kila kitu.
[8.42] Kumbukeni pale mlipo kuwa nyinyi kwenye ng'ambo yakaribu ya bonde, na wao wakawa ng'ambo ya mbali, namsafara ulipo kuwa chini yenu. Na ingeli kuwa mmeagana mngeli khitalifiana katika miadi. Lakini(mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo liliokuwa lazima litendeke, kwa sababu aangamie wakuangamia kwa dalili zilizo dhaahiri, na asalimike wakusalimika kwa dalili zilizo dhaahiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
[8.48] Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, naakawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo, nahali mimi ni mlinzi wenu. Yalipo onana majeshi mawili,akarudi nyuma, na akasema: Mimi si pamoja nanyi. Miminaona msiyo yaona. Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, naMwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.
[8.72] Hakika wale walio amini na wakahama na wakapiganiaNjia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, nawale walio toa mahala pa kukaa, na wakanusuru, hao ni marafiki na walinzi wao kwa wao. Na wale walioamini lakini hawakuhama, nyinyi hamna waajibu waulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame. Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia,isipo kuwa juu ya watu ambao yapo mapatano baina yenuna wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.