[9.3] Na ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtumewake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Munguna Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina. Basi mkitubu itakuwa kheri kwenu, na mkigeuka basijueni kuwa nyinyi hamumshindi Mwenyezi Mungu. Nawabashirie makafiri kuwa watapata adhabu chungu.
[9.24] Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu,na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, nabiashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko MwenyeziMungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basingojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.
[9.36] Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezikumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangualipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basimsidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikinawote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwaMwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu.
[9.37] Bila ya shaka kuakhirisha (miezi) ni kuzidi katikakukufuru; kwa hayo hupotezwa walio kufuru.Wanauhalalisha mwaka mmoja na kuharimisha mwaka mwingine, ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi)aliyo itukuza Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo huhalalishaalivyo viharimisha Mwenyezi Mungu. Wamepambiwa ubaya wa vitendo vyao hivi. Na Mwenyezi Munguhawaongoi watu makafiri.
[9.40] Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi MwenyeziMungu alikwisha mnusuru walipo mtoa walio kufuru, nayeni wa pili katika wawili walipo kuwa katika pango, naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike.Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Mwenyezi Munguakamteremshia utulivu wake, na akamuunga mkono kwamajeshi msiyo yaona, na akalifanya neno la waliokufuru kuwa chini, na Neno la Mwenyezi Mungu kuwa ndilo juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenyenguvu Mwenye hikima.
[9.69] Ni kama wale walio kuwa kabla yenu. Walikuwa wananguvu na mali na watoto zaidi kuliko nyinyi. Basiwalistarehea fungu lao, na nyinyi mnastarehea fungu lenu, kama walivyo starehe kwa fungu lao wale waliokuwa kabla yenu. Na nyinyi mkazama katika maovu kamawao walivyo zama. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika katika dunia na Akhera; na hao ndio waliokhasiri.
[9.70] Je, hazikuwafikia khabari za walio kuwa kabla yao- kaumu ya Nuhu, na A'ad, na Thamud, na kaumu yaIbrahim, na watu wa Madyana, na miji iliyo pinduliwa chini juu? Mitume wao waliwafikia kwa hoja zilizowazi. Basi Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu,walakini wao walikuwa wakijidhulumu wenyewe.
[9.74] Wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hawakusema; naowamekwisha sema neno la ukafiri, na wakakufuru baadaya kusilimu kwao. Na wakajihimu kufanya ambayo hawakuweza kuyafikia. Na hawakuchukia ila kuwaMwenyezi Mungu na Mtume wake amewatajirisha kutokanana fadhila zake. Wakitubu itakuwa kheri kwao, na wakigeuka Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu chunguduniani na Akhera. Na wala hawana katika ardhi mlinziwala wa kuwanusuru.
[9.99] Na katika Mabedui wapo wanao muamini MwenyeziMungu na Siku ya Mwisho, na wanaitakidi kuwa wanayoyatoa ndiyo ya kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu na ya kuwapatia dua za Mtume. Naam! Hayo ni kweli mambo yakuwasogeza. Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehemayake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mwenye kurehemu.
[9.111] Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsizao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapiganakatika Njia ya Mwenyezi Mungu - wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Hakikatika Taurati na Injili na Qur'ani. Na nani atimizaeahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzukukubwa,
[9.118] Na pia wale watatu walio achwa nyuma hata duniawakaiona dhiki juu ya ukunjufu wake, na nafsi zaozikabanika, na wakayakinika kuwa hapana pa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwake Yeye. Kishaakawaelekea kwa rehema yake ili nao waendelee kutubu.Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea toba naMwenye kurehemu.
[9.120] Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio jiranizao kubakia nyuma wasitoke na Mtume, wala kujipendeleanafsi zao kuliko yeye. Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa ajili yaNjia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapowaghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kuwa ni kitendochema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya mema.